MWALIMU ATEKWA, AFANYIWA UNYAMA JIJINI ARUSHA

Hii ndio document ya mwalimu huyo.
SIKILIZA KISA KINACHOFICHUA TUHUMA ZA MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA KAHAMAMIA NA MBUNGE WA VITI MAALUM (CCM) CATHERINE MAGIGE WAKIUSISHWA NA UTEKAJI, KULISHA SUMU, KUJERUHI NA KISHA KUMVUA VYEO MRATIBU ELIMU NGARENARO.
Tuesday, 11 0ctober, 2016

 Sikiliza hili tukio, Anaanza kusimulia.....

"Kwa majina naitwa Batuli Hamad Isaya , ni mwalimu wa Shule ya Msingi Unga Ltd ,kata ya unga Ltd Mkoani Arusha.

Nakumbuka ilikuwa siku ya jumatatu tarehe 3 jioni mida ya saa moja ,nilikuwa naenda dukani kununua vocha yangu ilikata.Kwa hiyo nikachukua hela nkaenda dukani .Nimefika dukani nikanunua vocha nikaikwangua nikawa narudi nyumbani.

Kutoka barabarani mpaka nyumbani kwangu kuna uchochoro ambao ni mrefu kidogo,nikawa naingiza vocha.Nlivyofika katikati ya uchochoro kuna mkaka alikuwa nyuma yangu ,akanisalimia ,anambia Batuli mambo ?nkamwambia poa .

Sikuhangaika naye kwa sababu niliona ni mtu anayenifahamu.Lakini ghafla,kwa dakika moja akaniambia simama hapo ulipo na ufuate maelekezo yangu ,tofauti na hapo nitakupiga shaba.

Nilipata hofu nikawa nimetetemeka ghafla simu yangu ikawa imedondoka lakini aliniambia okota simu yako .Akawa ametoa bastola amenishikia kwa mgongoni.

Baada ya hapo nikawa nimesimama kwa hofu nimetetmeka ,akaniambia usiogope,,Mimi nahitaji tu kuongea na wewe.Nitachokuelekeza ukifuate tofauti na hapo nitakupiga shaba ya kichwa.

Utarudi ulipotoka kuna gari jekundu ,utaingia kwenye hilo gari nataka tuzungumze.
Basi kwa ile hofu niliyokuwa nayo na kutetemeka niligeuka na kuanza kufuata maelekezo aliyonielekeza lakini alikuwa yuko nyuma mimi mbele.Nikaanza kurudi.

nikarudi mpaka barabarani nikateremka chini kidogo kwenye hilo gari nikafika ,akafungua mlango ,akaniambia niingie,kulikuwa na mkaka alikuwa amekaa ndani ya gari akanipisha nikakaa.Akafungua mlango yeye akazunguka upande wa dereva akapanda.

Ndani ya gari taa zilikuwa zimezimwa lakini kulikuwa kuna wakaka wawili,mmoja alikuwa alionipisha na mwingine alikuwa amekaa upande wa kushoto nikawa nimekaa katikati yao.
Baada ya muda ,yule kaka akawasha gari,akageuza akawa anaelekea upande wa juu.
Nikawa na hofu sana ,lakini aliyekuwa amekaa upande wa kulia kwangu akaanza kunisemesha ,we" Batuli,ulipoenda kumshtaki Mkuregenzi wako uache mara moja

.Na hapo ulipoenda kulalamika usirudi tena,kama unapenda kazi yako" .Tulia ufundishe na unyamaze ufunge mdomo kimya.

Wakati huo tulikuwa tumefika eneo moja lina mataa panaitwa Kona ya Esso.Nikawa nimeshtuka sana nikaendelea kupata hofu .Sasa baada ya kuniambia yale maneno ,nikawa nimepata wazo .

Au ni kwa sababu nilienda kulalamika kwa Mkuu wa Wilaya kuhusu inshu ya Mkuregenzi .Kwa hiyo nikawa najiuliza maswali kichwani.Lakini baada ya hapo nikaanza kuhisi siko salama .Nikaanza kupiga kioo cha gari.

Wakati huo tulikuwa tumefika eneo moja naiona sheli kwa mbele nafikiri ni maeneo ya kona mbauda.

Nikawa napiga lile gari kwa nguvu upande wa kulia ,kioo kikawa kimevunjika kwa malengo kwamba nipige sasa niombe msaada .Lakini wakati nagonga lile gari,kioo kilivyovunjika ,yule aliyekaa kulia kwangu akawa ameniwekea kiwiko cha mkono shingoni.

Alivyoniwekea kiwiko cha mkono shingoni akawa amenikandamiza,nikawa najitahidi kutoa ule mkono lakini akawa kama vile ananisukuma kichwani,akachukua kitambaa akaniziba pua na mdomo .Baada ya muda nikawa nimeishia kwenye usingizi.Kwa hiyo sikujua tena kilichoendelea.

Lakini baadae,nikawa nahisi tena niko kwenye gari ,nasikia sauti za watu wanaongea ,Nikajaribu kufumbua mdomo naona mdomo ni mzito .

Ile kufungua nikukutana kuna mkaka alikuwa amekaa pembeni yangu ambaye ni Askari lakini ninamfahamu anaitwa Yuda.Alikuwa amekaa pembeni ya kitanda ni mazingira ya hospital .Wakati huo kulikuwa kuna dokta ananicheki.

Basi wakati nimefungua macho,Yuda alikuwa anaendelea kunihoji ,ilikuwaje nikawa namueleza kwamba kulikuwa kuna watu wamenichukua wamenieleza moja mbili tatu.Wakati Yuda ananihoji dokta akawa anaendelea kunichoma dripu na amenichoma na sindano ndio wakati huo Yuda akawa anamueleza daktari kwamba kuna mabomba haya ya sindano tumeyakuta hapo chini ,wakawa wanayacheki baadaye dokta akasema kwamba haya mabomba ,hii kiboksi mlichokiokota ni kiboksi cha insulin,itakuwa wamemchoma dawa ya sukari kuteremsha sukari mpaka chini.

Na hapo hapo wakachukua vipimo wakanicheki sukari wakakuta kweli sukari iko chini wakaendelea kunitundikia dripu .Nikapelekwa wodini ,baadae dokta alinicheki akaniambia sijaingiliwa kwenye maumbile yangu ya kike lakini nilikuwa nableed.Nikamuuliza hii bleed inasababishwa na nini akaniambia ni hali ya hofu ndio maana bleed inatoka lakini hakuna jeraha lolote.

Ila kwa upande wa tumboni kulikuwa na maumivu makali ,kulikuwa na kijeraha ambacho kinaonekana nimechomwa na kitu chenye ncha kali,lakini manesi walivyonicheki wakasema kwamba hata ni kisu au bisibisi ,hajaingia sana ni kisehemu kidogo kama robo sentimeta .Nikaingizwa wodini nikaendelea kupata matatibu .Nikalala pale wodini mpaka asubuhi.

Asubuhi daktari akapita akanicheki nilikuwa na maumivu sehemu za tumbo,akaniandikia kwamba nitafanyiwa ultra sound lakini akanianzishia kwanza antibiotic, na baadae wakanichukua vipimo vya kunicheki maambukizi kwa sababu nilichomwa na vitu vyenye ncha kali mkononi pamoja na maeneo ya tumbo .Wakanicheki na HIV tes baadaye counselling nikafanyiwa counselling ,wakanishauri nianze kutumia dawa za kuzuia maambukizi kwa sababu damu yangu ilikuwa negative.

Nikakubali nikaanza hizo dawa ,wakanishauri nilale tena kwa siku ya pili ili waangalie kama mwili wangu utakuwa na mabadiliko yoyote .

Kwa hiyo nikabaki pale hospital ya Mt.Meru mpaka siku iliyofutilia asubuhi ,nikawa niko vizuri lakini asubuhi daktari akanishauri niendelee kutumia hizi dawa nisifanyiwa ultrasound.

Kama nitaonekana nina tatizo lolote basi nitarudi kwa ajili ya vipimo zaidi. Kwa hiyo akaniandikia dawa za kumeza antibiotic, wakanipa na hizo dawa ambazo nilikuwa nimeshazianza jana yake nikaruhusiwa kwenda nyumbani,

Naomba radhi stori ni ndefu naishia hapa, subili nitakuwekea Audio usikilize full stori. plz subiri 

No comments

Usisaau ku like